Mwaka 2000 hadi sasa na kuendelea, waTanzania wameonesha uhitaji wa kuishi kisasa kufuatia maendeleo ya tehama duniani, pia serikal zilizopita na iliopo madarakani kwa pamoja zimeonesha nia ya kutaka kumsaidia mtanzania kumiliki au kuishi katika makazi bora na yenye hamasa.
watanzania wengi hukumbwa na changamoto ya gharama za ujenzi na kwa maeneo ya miji hata upatikanaj wa viwanja pia umekua changamoto kubwa.
kutokana na changamoto hizo njia mbalimbali zimefanyika katika maeneo mbalimbali na hivyo baadhi ya watanzania wamenufaika kwa kiasi katika maeneo machache nchini.
Blog hii ime nuia kukuunganisha mtanzania wa hali.yoyote ya uchumi na mashirika, taasisi au makampuni yenye malengo yakusaidia kuboresha makazi kwa watanzania.
pia wewe mtumiaji wa mitandao ya kijamii unaweza boresha makazi ya Mtanzania kwa kutoa taarifa mbalimbali za majengo yanayo kodishwa au kuuzwa na gharama zake, vifaa mbalimbali vya ujenzi na gharama zake, viwanja na sehem vilipo na kuunganishwa moja kwa moja na eidha mteja au muuzaji wa kiwanja katika eneo husika kwa kuwasiliana na blogger wa MAKAZI MTANZANIA blog.
kwa kufanya hivyo itasaidia kupata taarifa zote za kuhusu uboreshaji wa makaz kwa watanzania pia kuisaidia serikali kufikia azima yake ya kuboresha makazi na huduma za jamii katika makazi husika.
MAKAZI TANZANIA pia itakuunganisha na makampuni au mashirika mbalimbali yanayo toa mikopo inayo lenga kuboresha makazi ya watanzania wenye hali mbalimbali za kifedha
mwisho utapata ushauri mbalimbali unao husu masuala ya maendeleo ya ardhi nchi nzima, upangaji, upimaji,ujenzi na taarifa mbalimbali za mazingira nchini kote.
kwa pamoja tunaweza, boresha makazi yako sasa
No comments:
Post a Comment