

1.UPANGAJI WA ARDHI
(SPATIAL
PLANNING/URBAN PLANNING)
Maana ya upangaji wa Ardhi ni pamoja na uandaaji wa michoro
ya ubunifu ya mipango miji ya maeneo ambayo itaratibu uendelezaji wa mji
husika.(inaitwa town planning drawings inshort TP), Kubadilisha matumizi ya
ardhi ya viwanja ambavyo vimeshapewa hati, Kutoa vibali vya ujenzi wa majengo, Kutoa
vibali vya upimaji wa Ardhi, Kufanya marekebisho ya michoro ya mipango miji
Mchoro wa mipango miji ambao unaonyesha matumizi mbali mbali ya eneo husika e.g
shule, open spaces etc ukishatayarishwa na manispaa ni lazima upelekwe wizarani
kwa mkurugenzi wa mipango miji wa wizara ya ardhi ili audhinishe.
Pia kitengo hiki cha upangaji kimeboreshwa Zaidi kwa
kushirikisha sekta binafsi katika upangaji na uboreshaji wa miji nchi, hata
hivyo sekta binafsi zmeweza kuisaidia serikali katika kuboresha miji mingi hapa
nchini kwa kuandaa mipango kabambe(master plan) katika mikoa mbalimbali na
hivyo kuongeza mazingatio katika uendelezaji wa miji nchi kote
2.
UPIMAJI ARDHI (LAND SURVEYING)
Maana ya upimaji Ardhi ni pamoja na kuweka
mawe yan Beacpon na kuonyesha mipaka ya maeneo yalio pimwa ,
Kazi kubwa ya mpimaji ni kupima eneo
ambalo tayari lina mchoro wa mipango miji na anatakiwa kupima kulingana na
mchoro wa mipango miji kama unavyo eleza na kazi hii hufuata baada ya upangaji
kukamiliaka yaani uandaaji wa mchoro(TP) wa eneo husika.
Upimaji huendana na mambo yafuatayo
· Kupanda mawe(beacons)
· Kutoa namba ya kiwanja/
eneo lililopimwa(plot number)
· Kuonyesha ukubwa wa
eneo (plot area)
· Kuonyesha mipaka ya kiwanja(plot boundaries)
· Kuandaa Ramani ya upimaji inayo onyesha mawe ya kiwanja,
kiwanja namba, ukubwa wa kiwanja na mipaka ya kiwanja ambayo lazima iwe
imesajiliwa na kuidhinishw na mkurugenzi wa upimaji na ramani wa wizara ya Ardhi
3.
UMILIKISHAJI WA ARDHI
Jukumu hili hufanywa na kitengo cha maafisa Ardhi kwa
kushirikiana na Tume ya umilikishaji Ardhi kanda kwa niaba ya wizara ya Ardhi, pia
kitengo cha umilikishaji Ardhi kina kazi ya Kuandaa hati miliki ya viwanja
ambavyo vimeshapimwa na ili aanze kukuandalia hati utatakiwa umpelekee mchoro
wa mipango miji unaonyesha kiwanja chako ili ajue matumizi yake, ramani ya
upimaji ya kiwanja chako ili ajue anaanda hati ya kiwanja gani, kipo wapi na
kina ukubwa gani hii husaidia wanapokadiria kodi ya kiwanja lazima wajue ukubwa
wa kiwanja, Kazi nyingine ya kitengo hiki ni kuhuisha miliki yani kuongeza mda
wa umilikiwa ardhi mana kuna hati za miaka 33, 66 na 99. Kazi nyingine ni
kuhamisha miliki kutoka kwa mmiliki mmoja na kwenda kwa mwingine inaitwa
transfer. Hati nayo ikisha kamilika kuandaliwa na manispaa au halmashauri ni
lazima ikahakikiwe na kamishna wa ardhi wa Kanda kwa niaba ya wizara na hatimaye
msajili wa hati naye ataisajili.
mara nyingi gharama
za kufanya yote hayo kwa sekta binafsi zinategemea wingi wa watu wanaohitaji
kupangiwa na kupimiwa maeneo yao hata hivyo kwa makubaliano kati ya mteja na
kampuni husika, wizara ya Ardhi kupiatia bodi ya mipango miji imeidhinisha
makampuni 33 mpaka kufikia mwezi Agast, 2016 yatakayo shiriki kupanga miji na
kufikia malengo ya kutoa hati nyingi Zaidi mpaka kufikia mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment