Tuesday, 4 October 2016

NINI MAANA YA MAKAZI HOLELA?

UTANGULIZI
Makazi holela ni aina ya maendeleo ya ardhi yasio fuata utaratibu maalum ulio panga eidha na serikali au kikundi cha watu fulani,
Aina hii ya maendeleo ya ardhi ilianza mara tu baada ya binadam kuanza maisha ya kujitafutia chakula na malazi, hata hivyo kwa historia kipindi hicho cha binadam kuanzisha makazi ni mara baada ya ugunduzi wa moto na baadae ugunduzi chuma.
Hata hivyo, upembuzi yakinifu kuhusu maendeleo holela ya matumizi ya ardhi huja kutokana na kukosekana kwa usimamizi wa taratibi maalum za mipango ya matumizi bora ya ardhi na hii imetokea maeneon mbalimbali katika nchi nyingi duniani.
MAKAZI HOLELA KATIKA BARA LA ULAYA
Maendeleo holela ya ardhi katika bara la ulaya yalikua kwa kasi kubwa kipindi cha mapinduzi ya viwanda miaka ya 1850 na hata kupelekea kuanza kwa taaluma ya upangaji wa mitaa ili kuboresha hali ya makazi ya bara hilo, pia hali hiyo ilizidi kuongezea katika mabara mengine likiwemo bara la Africa.
kutokana na kukua na kuongezeka kwa uhitaji wa makazi ya wanachi katika nchi mbalimbali barani Afrika, ikiwemo Tanzania, kulipelipelekea ongezeko kubwa la ujenzi usio rasmi yani makazi holela, ambayo kwa namna moja au nyingine yameongeza kasi ya matumizi ya ardhi nchini
Nikirudi katika maana halisi ya makazi holela nchini, makazi holela yamekua yakiongezeka kadili siku zinavyozidi kwenda mbele
Maeneo yenye Makazi holela mara nyingi hua na huduma duni za jamii kama vile Zahanati, shule, maji, barabara, mifereji ya maji taka na maeneo ya utunzanji taka ngumu, lakini pia yamekua na nyumba zilizo chini ya kiwango na hatarishi kwa uhai wa wakazi wa nyumba husika, wakati mwingine makazi haya yanatokea katika maeneo yasio salama kwa maisha ya binadamu kama vile pembezoni mwa mito au milima ambayo hua inaporomoka mara tu inapopatwa na majimaji kipindi cha mvua, ikumbukwe maafa mengi hutokea kwa wakazi wa maeneo haya na kugharimu maisha au gharama kubwa ya serikali katika kusaidia jamii na kaya zilizo athirika.
SHUGHURI ZA KIUCHUMI KATIKA MAKAZI HOLELA
Mara nyingi katika makazi haya, hua kuna tatizo la maeneno ya masoko na viwanda pia maeneo ya kufanyia biashara ndogondogo na kupelekea ongezeko la umasikinin katika makazi haya ingawaje kwa upande mwingine maeneo haya hukaliwa na watu wanye uwezo mkubwa kifedha na hua wanajenga majengo makubwa na ya thamani kubwa.
ATHARI ZA ONGEZEKO LA MAKAZI HOLELA
1. Kuongeza kasi ya umasikini kwa jamii husika kwa kukosa maeneo maalum ya kujishughurishia kazi zao binafsi za kiuchumi
2. Kuibuka kwa magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindipindu na marelia kutokana na ukosefu wa maeneo ya kutunza taka ngumu na mifereji ya maji machafu
3. Kuikoseha serikali mapato yanayotokana na kodi ya ardhi ambayo mara nyingi hutolewa kwa uthaminishaji wa maeneo yalio pimwa
4. Uharibifu wa mazingira unaotokana na uvamizi wa maeneo yasio stahili kuishi binadam na hivyo kupelekea upotevu wa baadhi ya viumbe hai
5. Nchi kuwa na muonekanao mbaya usiovutia na hupelekea kuathiri utalii wa nje
6. Ukosefu wa maeneo ya biashra, viwanda na masoko hupelekea nchi kukosa wawekwzaji wa nje
7. Kuzuka kwa migogoro ya ardhi inayo sababishwa na tatizo la kutokua na mipaka inayotamburika( plot boundary conflict)

Monday, 26 September 2016

IJUE TAALUMA YA MIPANGO MIJI TANZANIA

 
Moja ya kazi za kitaalam tanzania ni pamoja na fani ya upangaji wa miji ambao huendana na taaluma za upimaji pamoja na ubunifu wa majengo katika eneo husika.
upangaji na upimaji wa miji nchini umekua ukizorota kulingana na hali ya siasa na uelewa mdogo miongoni mwa jamii za kitanzania, hata hivyo upimaji na upangaji wa miji unafaida kubwa kwa mustakanbali wa taifa kwa ujumla katika nyanja mbalimbali zikiwemo za utunzaji mazingira, udhibiti wa matumizi bora ya ardhi, eundelezaji makazi kwa kuzingatia sheria pamoja na utengenezaji na ubunifu wa njia mbalimbali za kukuza uchumi kama vile utengaji maeneo ya ujasiliamali, viwanda, uekezaji na biashara.
siku za hivi karibuni taaluma hii imekua ikionekana kua na umuhimu mkubwa sana hasa kutokana na ongezeko la makazi holela katika majiji nchini: nitaeleza kwa uchache hali ilivyo kua katika majiji hayo
Tanzania tuna majiji makuu matono yani Dar es salaam, Arusha, Tanga, Mwanza na Mbeya, 
Makazi holela jijini Dar es salaam yamekua kwa kasi kubwa kuanzia miaka ya 2000, hata hivyo makazi mengi yameboreshwa kwa kiasi kidogo sana kwa kutoa nafasi za huduma zajamii, maeneo hayo ni kama vile Hananasifu, Vingunguti, Buguruni, Tabata, Mtoni, na Magomeni pia yapo maeneo mengi sana ambayo yanahitaji kufanyiwa uharaka ili kueza kutoa huduma za jamii walau kwa kiasi kidogo, maeneo hayo ni kama vile Mlalakua.
maeneo mengi yanayo fanana na hayo yamekua yakiongezeka pia katika maeneo ya majiji mengine hapa Tanzania.
hivyo kumbe taaluma hii inapaswa kupewa uzito wa aina yake hapa nchini ili kutatua na kumaliza kabisa swala la makazi holela na kuboresha muonekano wa nchi yetu
FURSA KWA WALIOSOMA TAALUMA HII
Chuo kikuu ardhi kilichopo jijini Dar es salaam ni miongoni mwa vyuo vikuu Barani Africa vinavyo toa wahitimu wapatao 100 kila mwaka wa fani ya upangaji wa miji na zaidi ya 150 wa fani nya upimaji ardhi, kutokana na uhitaji wa taaluma hii katika taifa letu ambao umepewa kipaumbele na serikaali ya awamu ya tano nchini, wahitimu zaid wanahitajika kutatua changamoto zote zinazotokea katika makazi ya jamii zetu, hata hivyo fursa hii kwa wahitimu haina ulazima wa kusubiri kuajiriwa na serikali au kampuni binafsi, ila wanaweza kuungana wenyewe na kutafuta kazi katika jamii popote nchini na waunganishe nguvu na wataalamu walio sajiriwa ili kuweza kupata usajiri wa kazi zao yani kupata kibali cha kupitisha michoro ya mipango wizarani kwa kufanya hivyo itasaidia makazi mengi nchini kupangwa na kupimwa na kuboresha matumizi ya ardhi.