Sunday, 25 September 2016

IJUE HALI YA MILIKI(REAL ESTATE) ILIVYO SASA TANZANIA





Real Estate(miliki) nchini Tanzania ni sekta inayokua kwa kasi sana kulinganisha na miaka ilio pita, kufikia mwaka 2016 ongezeko la nyumba 200,000 huhitajika kwa mwaka na hii inasababishwa na ukuaji wa idadi kubwa ya watu ambao wana kadiriwa kufikia milioni 45, hata hivyo kwa taarifa zilizo tolewa na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na uboreshaji wa makazi nchini zinaonesha kua kuna hitajiko la nyumba zaid ya million 3,  pamoja na juhudi kubwa sana zinazofanywa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, lakini bado kuna uhitaji mkubwa wa nyumba za makazi na biashara.




Kufuatia ongezeko hilo la mahitaji, Taasisi, mashirika na makampuni ya umma na binafsi yanayojihusisha na  uwekezaji ya ndani na nje ya nchi yameonesha uhitaji wa kuekeza kwenye sekta ya real estate (miliki) kwa kiasi kikubwa sana, mfano wa taasisi hizo ni zile za mafao ya jamii kama PSPF, NSSF, PPF, LPF, GEPF ambazo zote hizo zimewekeza katika sekta hii na kuonesha dalili ya kutaka kutatua tatizo la uhitaji wa makazi yapatao nyumba 200,000 kwa mwaka 2016. Lakini pia wawekezaji Zaidi wanapewa fursa ya kuendeleza sekta hii changa ya real estate katika mikoa yote nchini




SOKO LA REAL ESTATE TANZANIA



Kulingana na ukuaji na ongezeko la fursa mbalimbali za kibiashara katika majiji mbalimbali nchini, soko la real estate kwa maana nyumba za kuishi na zile za kibiashara zimezid kuongezeka siku hadi siku na hii ni fursa kwa sekta binafsi kuongeza juhudi katika uwekezaji wa sekta hii ambayo faida yake ni ya kudumu.




 FURSA KWA VIJANA NA WAHITIMU WA CHUO



Sekta hii sasa imekua ikiendeshwa na watu wasiokua na utaalam nayo wanaofahamika kama “madalali” ambao kwa namna moja au nyingine wamekua wakisababisha migogoro mikubwa katika jamii kutokana na ufahamu mdogo wa sekta hii, hivyo basi kulingana na uhitaji wa wataalam wa sekta hii katika jamii, kwa wahitimu wa vyuo wa sekta ya real estate ni muda muafaka sasa kuanza kutoa huduma hii kwa kuunganisha wamiliki wa nyumba za makazi na za biashara wahitaji wa nyumba hizo na upo uwezekano mkubwa wa kuanza kutoa huduma hii bila kua na mtaji au kua na mtaji mdogo kabisa.




“usikose kufuatilia Makala zangu katika mtandao huu ili kujua namna ya kuanza kutoa huduma za real estate bila kuwa na mtaji au kuwa na mtaji mdogo, ukakuza kipato chako kwa muda mrefu”





Toa maoni yako hapa 




No comments:

Post a Comment