Thursday, 22 September 2016

URASIMISHAJI WA MAKAZI HOLELA NCHINI UNAENDELEA KWA KASI KUBWA, PIA NI FURSA KWA WAHITIMU WA FANI ZA UPANGAJI NA UPIMAJI KUKUZA FANI ZAO NA KUTENGENEZA KIPATO ZAID


Kutokana na tatizo la maendeleo ya makazi holela nchi, SERIKALI inaendelea kuhakikisha inatoa hatimiliki zaidi ya 25,000 kwa wakazi wa kata za Kimara na Saranga zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kurasimisha makazi holela.
Hayo yalisemwa na Mratibu wa Mradi wa urasimishaji wa makazi holela Kata za Kimara na Saranga, Bi Grace Masatu wakati wa zoezi la ukaguzi wa maeneo ya mradi jijini Dar es salaam
“Zoezi za la upimaji linaenda sanjari na utambuzi wa mipaka,ujazaji wa madodoso, uchoraji wa ramani za upimaji na mipangomiji,”alisema Masatu.
Viwanja zaidi ya 25,000 vinatarajiwa kupimwa katika kata za Kimara na Saranga ambapo hadi leo ramani za upimaji 14 na ramani sita (6) za mipangomiji zenye jumla ya viwanja1028 ziko tayari na zimeshawasilishwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajli ya kupitishwa, alisema Masatu.
Aidha, Masatu amesema kuwa malengo ya mradi huo ni kuongeza thamani ya makazi kwa kutoa hatimiliki na kutambua mipaka ya wakazi wa maeneo husika.
Kwa upande wake, Afisa Mipango miji Mkuu, Bi Anna Macha, alisema kuwa hadi sasa maeneo yaliyopimwa katika kata ya Kimara ni mtaa wa Kilungule A wote pamoja na viwanja 724 vya mtaa wa Kilungule B, ambavyo vimechukuliwa mahesabu ya upimaji kwa ajili kuandaa ramani.
Ameongeza kuwa umetengenezwa mfumo maalum ambao unachukua taarifa za madodoso zinazojazwa wakati wa utambuzi wa mipaka ya wamiliki wa maeneo husika. Mfumo huo utaunganishwa na mfumo wa Kamishna wa Ardhi (MOLIS) utakaorahisisha kufahamu idadi ya viwanja vilivyopimwa na kumilikishwa.
Naye Mjumbe wa Mtaa wa Kilungule B, Bwana Claud Misri Silayo ameonyesha kuridhishwa na zoezi zima la utambuzi na upimaji wa maeneo.
“ Nimefurahishwa na zoezi la upimaji kwani nitamiliki ardhi kisheria, kihalali na nitafaidika na ardhi ninayomiliki kwa sababu mwisho wa zoezi hili nitapata hatimiliki ambayo itaniwezesha kupata mikopo kwenye taasisi za fedha,”alisema Silayo.
Urasimishaji ni mwendelezo wa utambuzi wa makazi holela katika jiji la Dar es Salaam unaotekelezwa chini ya Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 pamoja na Sheria ya Mipangomiji Na.7 ya mwaka 2007.
      Pia serikali imeendelea kutoa vibali kwa sekta binafsi kushiriki moja kwa moja kwenye zoez la upangaji na upimaji wa ardhi nchini, hivyo miradi mingi inatajiwa kuanza kufanyiwa kazi nchi nzima, zoez hili ni endelevu mpaka mwaka 2025

Zoezi hili pia linatoa fursa mbalimbali kwa wanafunzi waliomaliza vyuo mbalimbali nchini kikiwemo chuo kikuu ardhi kinachotoa wahitimu wa upangaji na upimaji wa ardhi kushiriki kikamilifu katika zoezi la uboreshaji makazi nchini kote.

No comments:

Post a Comment