Sunday, 25 September 2016

IJUE HALI YA MILIKI(REAL ESTATE) ILIVYO SASA TANZANIA





Real Estate(miliki) nchini Tanzania ni sekta inayokua kwa kasi sana kulinganisha na miaka ilio pita, kufikia mwaka 2016 ongezeko la nyumba 200,000 huhitajika kwa mwaka na hii inasababishwa na ukuaji wa idadi kubwa ya watu ambao wana kadiriwa kufikia milioni 45, hata hivyo kwa taarifa zilizo tolewa na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na uboreshaji wa makazi nchini zinaonesha kua kuna hitajiko la nyumba zaid ya million 3,  pamoja na juhudi kubwa sana zinazofanywa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, lakini bado kuna uhitaji mkubwa wa nyumba za makazi na biashara.




Kufuatia ongezeko hilo la mahitaji, Taasisi, mashirika na makampuni ya umma na binafsi yanayojihusisha na  uwekezaji ya ndani na nje ya nchi yameonesha uhitaji wa kuekeza kwenye sekta ya real estate (miliki) kwa kiasi kikubwa sana, mfano wa taasisi hizo ni zile za mafao ya jamii kama PSPF, NSSF, PPF, LPF, GEPF ambazo zote hizo zimewekeza katika sekta hii na kuonesha dalili ya kutaka kutatua tatizo la uhitaji wa makazi yapatao nyumba 200,000 kwa mwaka 2016. Lakini pia wawekezaji Zaidi wanapewa fursa ya kuendeleza sekta hii changa ya real estate katika mikoa yote nchini




SOKO LA REAL ESTATE TANZANIA



Kulingana na ukuaji na ongezeko la fursa mbalimbali za kibiashara katika majiji mbalimbali nchini, soko la real estate kwa maana nyumba za kuishi na zile za kibiashara zimezid kuongezeka siku hadi siku na hii ni fursa kwa sekta binafsi kuongeza juhudi katika uwekezaji wa sekta hii ambayo faida yake ni ya kudumu.




 FURSA KWA VIJANA NA WAHITIMU WA CHUO



Sekta hii sasa imekua ikiendeshwa na watu wasiokua na utaalam nayo wanaofahamika kama “madalali” ambao kwa namna moja au nyingine wamekua wakisababisha migogoro mikubwa katika jamii kutokana na ufahamu mdogo wa sekta hii, hivyo basi kulingana na uhitaji wa wataalam wa sekta hii katika jamii, kwa wahitimu wa vyuo wa sekta ya real estate ni muda muafaka sasa kuanza kutoa huduma hii kwa kuunganisha wamiliki wa nyumba za makazi na za biashara wahitaji wa nyumba hizo na upo uwezekano mkubwa wa kuanza kutoa huduma hii bila kua na mtaji au kua na mtaji mdogo kabisa.




“usikose kufuatilia Makala zangu katika mtandao huu ili kujua namna ya kuanza kutoa huduma za real estate bila kuwa na mtaji au kuwa na mtaji mdogo, ukakuza kipato chako kwa muda mrefu”





Toa maoni yako hapa 




Thursday, 22 September 2016

MUONGOZO WA UPANGAJI, UPIMAJI NA UMILIKISHAJI ARDHI

Image result for picha za upangaji ardhiImage result for picha za upangaji ardhi


1.UPANGAJI WA ARDHI 
(SPATIAL PLANNING/URBAN PLANNING)
Maana ya upangaji wa Ardhi ni pamoja na uandaaji wa michoro ya ubunifu ya mipango miji ya maeneo ambayo itaratibu uendelezaji wa mji husika.(inaitwa town planning drawings inshort TP), Kubadilisha matumizi ya ardhi ya viwanja ambavyo vimeshapewa hati,  Kutoa vibali vya ujenzi wa majengo, Kutoa vibali vya upimaji wa Ardhi, Kufanya marekebisho ya michoro ya mipango miji Mchoro wa mipango miji ambao unaonyesha matumizi mbali mbali ya eneo husika e.g shule, open spaces etc ukishatayarishwa na manispaa ni lazima upelekwe wizarani kwa mkurugenzi wa mipango miji wa wizara ya ardhi ili audhinishe.
Pia kitengo hiki cha upangaji kimeboreshwa Zaidi kwa kushirikisha sekta binafsi katika upangaji na uboreshaji wa miji nchi, hata hivyo sekta binafsi zmeweza kuisaidia serikali katika kuboresha miji mingi hapa nchini kwa kuandaa mipango kabambe(master plan) katika mikoa mbalimbali na hivyo kuongeza mazingatio katika uendelezaji wa miji nchi kote

2.    UPIMAJI ARDHI (LAND SURVEYING)
 Maana ya upimaji Ardhi ni pamoja na kuweka mawe yan Beacpon na kuonyesha mipaka ya maeneo yalio pimwa ,
Kazi kubwa ya mpimaji ni kupima eneo ambalo tayari lina mchoro wa mipango miji na anatakiwa kupima kulingana na mchoro wa mipango miji kama unavyo eleza na kazi hii hufuata baada ya upangaji kukamiliaka yaani uandaaji wa mchoro(TP) wa eneo husika.
Upimaji huendana na mambo yafuatayo
·       Kupanda mawe(beacons)
·        Kutoa namba ya kiwanja/ eneo lililopimwa(plot number)
·        Kuonyesha ukubwa wa eneo (plot area)
·       Kuonyesha mipaka ya kiwanja(plot boundaries)
·       Kuandaa Ramani ya upimaji inayo onyesha mawe ya kiwanja, kiwanja namba, ukubwa wa kiwanja na mipaka ya kiwanja ambayo lazima iwe imesajiliwa na kuidhinishw na mkurugenzi wa upimaji na ramani wa wizara ya Ardhi

3.     UMILIKISHAJI WA ARDHI
Jukumu hili hufanywa na kitengo cha maafisa Ardhi kwa kushirikiana na Tume ya umilikishaji Ardhi kanda kwa niaba ya wizara ya Ardhi, pia kitengo cha umilikishaji Ardhi kina kazi ya Kuandaa hati miliki ya viwanja ambavyo vimeshapimwa na ili aanze kukuandalia hati utatakiwa umpelekee mchoro wa mipango miji unaonyesha kiwanja chako ili ajue matumizi yake, ramani ya upimaji ya kiwanja chako ili ajue anaanda hati ya kiwanja gani, kipo wapi na kina ukubwa gani hii husaidia wanapokadiria kodi ya kiwanja lazima wajue ukubwa wa kiwanja, Kazi nyingine ya kitengo hiki ni kuhuisha miliki yani kuongeza mda wa umilikiwa ardhi mana kuna hati za miaka 33, 66 na 99. Kazi nyingine ni kuhamisha miliki kutoka kwa mmiliki mmoja na kwenda kwa mwingine inaitwa transfer. Hati nayo ikisha kamilika kuandaliwa na manispaa au halmashauri ni lazima ikahakikiwe na kamishna wa ardhi wa Kanda kwa niaba ya wizara na hatimaye msajili wa hati naye ataisajili.

 mara nyingi gharama za kufanya yote hayo kwa sekta binafsi zinategemea wingi wa watu wanaohitaji kupangiwa na kupimiwa maeneo yao hata hivyo kwa makubaliano kati ya mteja na kampuni husika, wizara ya Ardhi kupiatia bodi ya mipango miji imeidhinisha makampuni 33 mpaka kufikia mwezi Agast, 2016 yatakayo shiriki kupanga miji na kufikia malengo ya kutoa hati nyingi Zaidi mpaka kufikia mwaka 2025.

TATHMINI YA UREJESHAJI WA ARDHI NA MASHAMBA KWA WANANCHI KUTOKA KWA WAWEKEZAJI NCHINI













Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imedhamiria kutatua tatizo la wawekezaji katika ardhi na mashamba
wasiokuwa na dhamira njema na maendeleo ya nchi hii.Hili limejidhihirisha dhahiri katika zoezi linaloendelea la kubaini maeneo husika na kuyabatilisha kutoka kwa wamiliki husika na kupatiwa wananchi kuyaendeleza sambamba na agizo la Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli.Hivi karibuni, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mheshimiwa William Lukuvi alizitaka halmashauri zote nchini, kufanya uhakiki wa mashamba makubwa ambayo hayajaendelezwa kwa muda mrefu na kutoa notisi kwa wamiliki wake ili wafahamu hatua zitakazochukuliwa na Serikali.Alisema hayo wakati akitangaza kwa wananchi wa Tanga kuhusu kufutwa kwa hati miliki ya mashamba matano ya mkonge yaliyopo wilaya za Muheza na Pangani. Mashamba hayo ni Lewa Estate, Kipumbwi, Azimio, Bwembwera na
Sakula.Mheshimiwa Lukuvi alisema; “Mheshimiwa Rais alifikia uamuzihuo Desemba 19, mwaka jana baada ya kujiridhisha kuwa wamiliki wake wameshindwa kuyaendeleza mashamba hayo kwa shughuli zilizokusudiwa kama walivyokuwa wameomba katika vijiji husika”.Mheshimiwa Lukuvi aliuagiza mkoa wa Tanga, upendekeze mali zilizopo kwenye mashamba hayo, kama majengo ya ofisi na mali nyingine
wapewe watu gani kwa ajili ya maendeleo ya eneo husika kabla mashamba hayo hayajagawiwa.
Pia, aliagiza kuwa mkoa lazima uhakikishe wamejua idadi kamili ya wananchi walioko katika mashamba hayo na kiasi cha ardhi iliyopo, ikiwepo kufanya utaratibu pia wa ulipaji wa fidia kwa wale
wanaostahili.Aidha, amani iliyokosekana kwa takriban miaka kumi katika Kijiji cha Kapunga wilayani Mbarali mkoa wa Mbeya, imerejea baada ya Mheshimiwa Lukuvi kuwatangazia wananchi kurejeshwa kwa hekta 1,870 zilizounganishwa kimakosa kwenye shamba la mwekezaji mwaka 2005. Awali mwaka 1985, Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, aliwaomba wakazi wa Kijiji cha Kapunga eneo lenye ukubwa wa hekta 5,500 ili kupata eneo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, na hasa kuboresha kilimo nchini. Wananchi walikubali ombi hilo la Mwalimu Nyerere na kutoa hekta hizo. Lakini, wananchi hao
wa Kapunga walishangazwa baadaye kuona kuwa hata yale maeneo waliyobaki nayo, yakafanywa kuwa ya mwekezaji ambaye ni Kampuni ya Export Trading Group, Katika kipindi hicho chote cha miaka kumi,
wananchi wa Kapunga wamekuwa wakipata matatizo ya aina mbalimbali katika eneo hilo, kwa Export Trading Group
kujichukulia maeneo mengine ya wananchi hao. Baadhi ya mateso
waliyopata kutoka kwa mwekezaji huyo ni kuvunjiwa daraja, kumwagiwa sumu katika mashamba yao n.k.
 Hatahivyo baada ya agizo la Rais la kumtaka mwekezaji huyo, kurejesha kiasi cha hekta 1,870wa wananchi, maeneo hayo sasa ni ya wananchi.
Mheshimiwa Lukuvi alitangaza; “Tumekaa na kukubaliana, kiasi hiki cha ardhi kirejeshwe kwenu na mwekezaji amekubali hekta hizo sasa ni mali ya kijiji chenu”.Zoezi limeendelea katika mikoa ya Morogoro na Tanga, ambapo hati za miliki za mashamba makubwa 13 yenye zaidi ya ekari 24,000, yaliyoagizwa na Mheshimiwa Rais Magufuli, zilifutwa na mashamba hayo kukakabidhiwa kwa wananchi wasio na ardhi. Serikali imetakiwa itenge maeneo mengine kwa ajili ya uwekezaji katika mikoa
hiyo, baada ya wamiliki wake kushindwa
kuyaendeleza.Mheshimiwa Lukuvi alisema: “Sheria ya vijiji inaruhusu vijiji kumilikisha ardhi isiyopungua ekari 50 kwa kuitisha mkutano wa kijiji ili uridhie, lakini baadhi ya viongozi wamekuwa wakishirikiana na wawekezaji matapeli ili wapewe ardhi kwa njia za hila”.
Vile vile akiwa wilayani Monduli mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Lukuvi alikabidhi ekari 39,924 za mashamba kwa wananchi, baada ya Mheshimiwa Rais Magufuli kufuta hatimiliki za wawekezaji 13.
Akiongea na wananchi wa kata za Lokisale na Olmoti katika mkutano wa hadhara, Mheshimiwa Lukuvi alisema; “Rais amefikia hatua hiyo baada
ya wawekezaji hao kushindwa kuyaendeleza
mashamba waliyokabidhiwa kwa ajili ya kilimo cha biashara na kuwaacha wananchi bila ardhi”. Kwa ujumla, Wizara ya Ardhi inaendelea
kushughulikia umilikishaji ardhi usiofuata sheria katika maeneo mengi nchini. Mathalani, katika wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara, wanakijiji wa Kilombero Kata ya Shambarai, wamerudishiwa ekari 828 za mashamba manne yaliyochukuliwa na familia moja baada ya kujimilikisha bila kufuata sheria. Familia ya watu wanne wa kijiji hicho,
walijimilikisha ekari 1,028 bila kufuata kanuni, taratibu na sheria za ardhi, hivyo wananchi hao wakawanyang’anya ekari 828 na kuwaachia ekari
200.Aidha, zaidi ya mashamba 35 yanatarajiwa
kubatilishwa milki na Serikali ndani ya mwaka huu 2016.

Source;: www.ardhi.go.tz