Monday, 26 September 2016

IJUE TAALUMA YA MIPANGO MIJI TANZANIA

 
Moja ya kazi za kitaalam tanzania ni pamoja na fani ya upangaji wa miji ambao huendana na taaluma za upimaji pamoja na ubunifu wa majengo katika eneo husika.
upangaji na upimaji wa miji nchini umekua ukizorota kulingana na hali ya siasa na uelewa mdogo miongoni mwa jamii za kitanzania, hata hivyo upimaji na upangaji wa miji unafaida kubwa kwa mustakanbali wa taifa kwa ujumla katika nyanja mbalimbali zikiwemo za utunzaji mazingira, udhibiti wa matumizi bora ya ardhi, eundelezaji makazi kwa kuzingatia sheria pamoja na utengenezaji na ubunifu wa njia mbalimbali za kukuza uchumi kama vile utengaji maeneo ya ujasiliamali, viwanda, uekezaji na biashara.
siku za hivi karibuni taaluma hii imekua ikionekana kua na umuhimu mkubwa sana hasa kutokana na ongezeko la makazi holela katika majiji nchini: nitaeleza kwa uchache hali ilivyo kua katika majiji hayo
Tanzania tuna majiji makuu matono yani Dar es salaam, Arusha, Tanga, Mwanza na Mbeya, 
Makazi holela jijini Dar es salaam yamekua kwa kasi kubwa kuanzia miaka ya 2000, hata hivyo makazi mengi yameboreshwa kwa kiasi kidogo sana kwa kutoa nafasi za huduma zajamii, maeneo hayo ni kama vile Hananasifu, Vingunguti, Buguruni, Tabata, Mtoni, na Magomeni pia yapo maeneo mengi sana ambayo yanahitaji kufanyiwa uharaka ili kueza kutoa huduma za jamii walau kwa kiasi kidogo, maeneo hayo ni kama vile Mlalakua.
maeneo mengi yanayo fanana na hayo yamekua yakiongezeka pia katika maeneo ya majiji mengine hapa Tanzania.
hivyo kumbe taaluma hii inapaswa kupewa uzito wa aina yake hapa nchini ili kutatua na kumaliza kabisa swala la makazi holela na kuboresha muonekano wa nchi yetu
FURSA KWA WALIOSOMA TAALUMA HII
Chuo kikuu ardhi kilichopo jijini Dar es salaam ni miongoni mwa vyuo vikuu Barani Africa vinavyo toa wahitimu wapatao 100 kila mwaka wa fani ya upangaji wa miji na zaidi ya 150 wa fani nya upimaji ardhi, kutokana na uhitaji wa taaluma hii katika taifa letu ambao umepewa kipaumbele na serikaali ya awamu ya tano nchini, wahitimu zaid wanahitajika kutatua changamoto zote zinazotokea katika makazi ya jamii zetu, hata hivyo fursa hii kwa wahitimu haina ulazima wa kusubiri kuajiriwa na serikali au kampuni binafsi, ila wanaweza kuungana wenyewe na kutafuta kazi katika jamii popote nchini na waunganishe nguvu na wataalamu walio sajiriwa ili kuweza kupata usajiri wa kazi zao yani kupata kibali cha kupitisha michoro ya mipango wizarani kwa kufanya hivyo itasaidia makazi mengi nchini kupangwa na kupimwa na kuboresha matumizi ya ardhi.